Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, tamko la kituo cha uongozi wa Hawza katika kuunga mkono ujumbe wa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu kutokana na mnasaba wa arobaini ya mashahidi, ni kama ifuatavyo:
بسم الله الرحمن الرحیم
«وَکَانَ حَقًّا عَلَیْنَا نَصْرُ الْمُؤْمِنِینَ»
Na ilikuwa ni haki juu yetu kuwanusuru Waumini.
(R'um: 47)
Chini ya mwanga wa maneno ya mwongozo wa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi (Mola amuhifadhi), mara nyingine tena amewahutubia wanawe wa Hawza, na katika kipindi cha vita vya kupandikizwa vya adui, amewaweka juu ya mabega ya wanawe wa kiroho nchini kote jukumu nyeti la kuleta utulivu na amani katika nyoyo za waumini na wapenzi, na kuhimiziana subira, kwa kuwa Amir al-Mu'minin Ali (as) aliliita jambo hili kuwa ni dhamana ya ushindi pale aliposema:
«اَلصَّبْرُ کَفِیلٌ بِالظَّفَر».
Na sasa, ni vyema wanafunzi na maulamaa watukufu wa Hawza, kwa kuiga mfano wa subira na ujasiri wa uwanda wa Karbala, waitikie wito wa kiongozi mwenye busara na hekima wa mapinduzi, na kama wanavyojua nafsi zao kuwa ni askari na watekelezaji wa maelekezo ya kiongozi huyo mwenye hekima, wakiwa pamoja na wananchi wenye ufahamu na vijana waumini, washikilie na kudumisha hamasa na uelewa wa kimapinduzi, na kwa kuhifadhi roho ya jihadi ya mapambano na ufafanuzi, washinde vita vya kupandikizwa na vya kimitandao vya adui katili wa kizayuni, na kwa fadhila za Mwenyezi Mungu, waandae mazingira ya kumuangamiza adui huyu mnywa damu na muuaji wa watoto.
Ni wazi kuwa maulamaa na wanafunzi wa Hawza wenye wivu wa dini na mapinduzi, sambamba na kufanya upya kwa kiapo na ahadi yao kwa Kiongozi wa Waislamu wa ulimwengu, wameupa thamani utekelezaji wa wajibu uliowekwa juu yao na Kamanda Mkuu wa Vikosi, na kwa kutoa nafsi zao hadi tone la mwisho la damu, kama alivyotaka yeye, watautekeleza kwa msaada wa Mwenyezi Mungu.
"وَ مَا النَّصْرُ إِلَّا مِنْ عِندِ اللَّهِ الْعَزِیزِ الْحَکِیمِ"
Kituo cha Uongozi wa Hawza.
Maoni yako